HabariMilele FmSwahili

Mawaziri waliopendekezwa kuanza kupigwa msasa leo

Margaret Kobia aliyependekezwa kuhudumu katika wizara ya utumishi wa umma vijana na jinsia atakuwa wa kwanza kufika mbele ya kamati ya uteuzi hivi leo kupigwa msasa. Kamait hiyo inayoongozwa na wabunge wa taifa spika Justin Muturi pia itawahoji John Munyes wa kawi, Monica Juma wa masuala ya nje na waziri mteule wa ardhi Farida Karoney. Muturi akiwahakikishia wakenya lalama zozote zilizowasilishwa dhidi yao zitaangaziwa. Zoezi la kuwapiga msasa wote hao litakamilika hapo kesho.

Show More

Related Articles