HabariPilipili FmPilipili FM News

Mawakili Wa Miguna Wataka Kujua kilichopelekea kusafirishwa Kwake

Mawakili wa Miguna Miguna bado wanataka kuelezewa kwa undani kuhusiana na kauli ya serikali kufutilia mbali uraia wa mwanaharakati wa NASA Miguna Miguna, na hatua ya kumsafirisha nchini CANADA bila mahakama kuarifiwa.

Akiongea mbele ya mahakama ya milimani ambako kesi ya kujua kilichopelekea kusafirishwa kwa miguna hadi nchini Canada inaendelea, wakili Mutula Kilonzo Junior ametaka kufahamu ni vipi tume ya IEBC ilimuidhinisha Miguna kuwania ugavana wa Nairobi iwapo yeye si raia wa Kenya.

Naye wakili JAMES Orengo amemtaka jaji wa mahakama hiyo Luka Kimaru kuhakikisha inspekta generali wa polisi Joseph boinet na George Kinoti wanafika mahakamani wakiandamana na Miguna kama walivyoamuriwa.

 

Show More

Related Articles