HabariPilipili FmPilipili FM News

Shughuli Za Uzalishaji Wa Nguvu Za Umeme Zahofiwa Kutatizika

Shughuli za uzalishaji wa nguvu za umeme nchini huenda zikatatizika kutokana na kushuka kwa Kiwango cha maji kwenye mabwawa ya kuzalisha nguvu za umeme nchini.

Charles Keter ambaye ni waziri wa Kawi nchini amebaini kuwa  endapo mvua haitanyesha ifikapo mwezi wa tatu basi huenda shirika la usambazaji nguvu za umeme nchini KPLC likalazimika kuanza mgao wa umeme kwa wakenya.

Hata hivyo Keter amewahakikishia wawekezaji katika miji mbali mbali nchini kuwa serikali, ina kawi ya kutosha kwa shughuli za uwekezaji inayozalishwa kupitia mfumo wa Geothermal huko maeneo ya Olkaria.

Show More

Related Articles