HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Idara ya polisi yakanusha njama ya kuwakamata viongozi wa NASA

Idara ya usalama sasa imesema haina haja wala sababu ya kuwatia mbaroni viongozi kumi na wawili wa muungano wa NASA ambao walifika mahakamani hii leo kuomba dhamana kuzuia kutiwa mbaroni.
Kwenye ujumbe kupitia mtandao wa twitter, idara ya polisi imesema viongozi hao pia hawana haja kufika katika kitengo cha ujasusi kuandikisha taarifa kwani kwa sasa hawatakikani kufanya hivyo.
Haya yanajiri huku idara ya uhamiaji ikisimamisha kwa muda matumizi ya Pasipoti za maafisa kadhaa wa NASA akiwemo James Orengo, Jimmy Wanjigi, David Ndii miongoni mwa wengine.

Show More

Related Articles