HabariMilele FmSwahili

Miguna Miguna afikishwa katika mahakama ya Milimani

Mwanasiasa Miguna Miguna amefikishwa katika mahakama ya Milimani hapa Nairobi. Hii ni baada yake kudinda kujibu mashtaka yanayomkabli katika mahakama ya Kajiado mapema leo. Miguna anafika mbele ya jaji Luka Kimaru aliyeagiza afikishwe mbele yake kusomewa mashtaka yanayomkabili. Yakijiri hayo,jaji wa mahakama kuu Roselyne Aburili amebatili uamzi wa idara ya polisi kumpokonya mbunge wa Homa Bay mjini Peter Kaluma silaha yake. Katika uazmi wake,jaji Abrili pia amebatili agizo la polisi kuwapokonya wabunge 141 walinzi wao.

Show More

Related Articles