HabariMilele FmSwahili

Miguna Miguna adinda kujibu mashtaka dhidi yake katika mahakama ya Kajiado

Mwanasiasa Miguna Miguna amedinda kujibu mashtaka dhidi yake katika mahakama ya Kajiado. Miguna aliyefikishwa katika mahakama hio mapema leo,anadai kesi yake inafaa kusikizwa na Jaji Luka Kimaru katika mahakama ya Milimani na wala sio Kajiado. Kulingana naye tayari jaji Kimaru ametoa agizo la kuwasilishwa kwake Nairobi na hivyo hatokubaliana na uamuzi wa kushtakiwa kwengine. Kwa sasa Miguna anazuiliwa katika jela ya mahakama hio ya Kajiado. Aidha mchana huu jajai Luka Kimaru anatazamiwa kutoa uamuzi wake kuhusiana na ombi la kuadhibiwa insepcta generali wa polisi Joseph Boinnet na mkuu wa idara ya jinai George Kinoti kwa kukosa kujisalimisha mahakamani mapema leo pamoja na Miguna kama walivyotakiwa.

Show More

Related Articles