HabariMilele FmSwahili

Gavana Nyong’o afika mahakamani kuishtaki serikali kwa kuondoa ulinzi wake

Gavana wa Kisumu Anyang’ Nyong’o amefika mahakamani kuishtaki serikali kwa kuondoa ulinzi wake. Nyongo na naibu wake Mathews Owili wanadai ni haki yao kukabidhiwa ulinzi huo. Tayari wabunge 141 wa NASA wamewasilisha kesi mahakamani kuhusiana na kupokonywa ulinzi wao. Wakili wao mbunge Peter Kaluma anataka mahakama kuishurutisha serikali kuwapa ulinzi kwani huenda maisha yao yakawa hatarini.

Show More

Related Articles