HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwanaume Afikishwa Mahakamani Kwa Kumpiga Jirani Yake

Mwanamume mmoja amefikishwa mbele ya mahakama ya Kwale kujibu shtaka la kumpiga na kumsababishia majeraha mama mmoja anayedaiwa kuwa jirani yake.

Inadaiwa  mnamo tarehe 29 mwezi Oktoba mwaka 2017 katika kijiji cha Dzimanya huko Vigurungani gatuzi dogo la Kinango mwanamme kwa jina Mrinzi Nyawa alimpiga  Christine Kiluvi na kumjeruhi.

Mbele ya Hakimu mkaazi Patric Wabungu mshtakiwa amekiri shtaka hilo akisema alifanya kitendo hicho kufuatia tofauti za kinyumbani.

Mahakama imemhukumu mwanamume huyo  kifungo cha miezi sita ama faini ya shilingi laki moja.

Show More

Related Articles