People Daily

Matatu Zitakazo Patikana Ziki Cheza Video Chafu Zita Chukuliwa Hatua Kali

Mratibu wa chama cha wenye matatu kanda ya Pwani Salim Mbarak ameunga mkono hatua ya bodi ya kudhibiti ubora wa filamu nchini KFCB kuanzisha msako dhidi ya matatu za abiria zinazocheza video za ukosefu wa maadili.

Akiongea na meza yetu ya habari, Mbarak amesema baadhi ya video zinazochezwa kwenye matatu hizo hapa Mombasa zinaenda kinyume cha dini na mila za kiafrika.

Amesema madereva watakaopatikana na hatia hiyo wanapaswa kushtakiwa.

Polisi na bodi ya KFCB walianzisha msako huo hapo jana ambapo matatu zinazolengwa ni za Tudor, Mtwapa, na Bamburi.

Show More

Related Articles