HabariPilipili FmPilipili FM News

Mkrugenzi Wa Mashtaka Ya Umma Atakiwa Kufika Mbele Ya Mahakama Kuu

Jaji wa mahakama kuu Luka Kimaru amemuagiza  mkurugenzi wa mashtaka ya umma kufika mbele yake leo saa sita mchana kuelezea iwapo mwanasiasa Miguna Miguna ameshitakiwa au la.

Hii ni baada ya kiongozi wa mashtaka Nicholas Mutuku kumwambia jaji Kimaru kwamba Miguna alifikishwa mapema leo katika mahakama ya Kajiado badala ya Milimani kama ilivyoagizwa jana.

Jaji Kimaru ameahidi kutoa uamuzi wake iwapo inspekta generali wa polisi Joseph Boinett na George Kinoti wa DCI wamekiuka agizo la mahakama baadaye mchana wa leo.

Show More

Related Articles