HabariPilipili FmPilipili FM News

Wamiliki Wa Maduka Waonywa Dhidi Ya Utumizi Wa Mifuko Ya Plastiki

Onyo kali limetolewa kwa wamiliki wa maduka Kwale wanaodaiwa  kuendeleza Biashara ya mifuko ya plastiki  iliyopigwa marufuku kuwa atakayepatikana atakabiliwa kisheria.

Afisa wa halmashauri ya mazingira NEMA tawi la kwale   Cicilia Nyambu ametoa onyo hilo baada ya kubainika kwamba bado kuna mifuko ya plastiki ambayo anadai imeingizwa humu nchini kutoka nchi jirani ya Tanzania na wafanyabiashara kinyume cha sheria za nchi.

Waliotajwa kutumia mifuko hiyo ni wachuuzi wa vibanda vya mboga mjini Kwale pamoja na maeneo mengine katika kaunti hiyo.

Aidha amekiri kukumbwa na changamoto ya kutekeleza sheria ya mifuko hiyo kutokana na kukosekana kwa maafisa wa kutosha kutekeleza zoezi hilo.

Show More

Related Articles