HabariK24 TvMakalaSwahiliSwahili VideosVideos

KIU MILIMANI: Uhaba wa maji unatishiwa pakubwa na uharibifu wa vyanzo

Je, kuna uwezekano kuwa Kenya inakodolea macho janga la ukosefu wa maji?
Uhaba wa maji haswa katika maeneo ya mijini umeshuhudiwa kila kuchapo na hakuna dalili za  hali hiyo kuimarika hivi karibuni huku ikizingatiwa kuwa ongezeko la watu mijini linashuhudiwa.
Ukataji miti na shughuli za ukulima katika maeneo ya vyanzo vya maji katika Mlima Kenya na Msitu wa Aberdare umekuwa ukiendelea lakini kulingana na shirika la huduma ya  misitu ukataji miti unaoendelea ni halali.
Katika makala maalum ya “kiu milimani” Dan Kaburu alizuru msitu wa Mlima Kenya na Aberdare kutathmini hali halisi ya mambo ambayo ni ya kutia hofu.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.