HabariMilele FmSwahili

Bernard Leparmarai ndiye mshirikishi wa usalama kanda ya Pwani

Bernard Leparmarai sasa ndiye mshirikishi wa usalama kanda ya Pwani wadhifa uliokuwa unaongozwa na Nelson Marwa aliyeteuliwa katika baraza jipya la mawaziri. Leparmarai aliyekuwa mshirikishi kaunti ya Nairobi sasa wadhifa wake utakabidhiwa William Thuku. Kwenye mabadiliko yaliyochapishwa na waziri wa usalama wa kitaifa dr Fred Matiangi, wadhifa wa mshirikishi kanda ya North Rift uliosimamiwa na Wanyama Musiambo aliyejiunga na baraza la mawaziri umekabidhiwa Mongo Chimwaga. Mabadiliko hayo yamefanyiwa kanda zote 8 nchini, japo Balozi Mohamed Saleh atasalia eneo la Kaskazini Mashariki. Mabadiliko mengine pia yamefanyiwa makamishna wa kaunti ambapo sasa Amos Mariba atakuwa kamishna wa kaunti ya Nairobi, Evans Achoki atasalia Mombasa na Pauline Dola atasimamia Kisumu.

Show More

Related Articles