BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Anaye Shukiwa Kumuua Mowzey Radio Atiwa Mbaroni

Wiki iliyopita  Nchi ya Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla iligumbikwa na huzuni baada ya taarika za kifo cha  mwanamziki Moses SseKibogo almaarufu kama Mowzey Radio.

Radio alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Case mjini kampala nchini Uganda kwa mda wa wiki mbili. Baada ya kupata jeraha la kichwa aliyoipata kupitia vuta ni kuvute  kati yake na walinzi wa Klabu moja mjini humo kabla ya kifo chake siku ya Alhamisi wiki iliyo pita.

Siku ya Jumapili  Maafisa wa polisi kutoka kituo cha Katwe walimkamata Jamaa mmoja kwa jina Godfery Wamala  aneye husishwa na kifo cha Mowzey.

Kilingana na Shirika la habari la New Vision Nchini Uganda Mshukiwa huyo alitiwa mbaroni akiwa nyumbani kwa rafiki yake alipo kuwa akijificha .

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.