HabariPilipili FmPilipili FM News

Muuzaji Mifuko Ya Plastiki Atiwa Mbaroni.

Mtu mmoa amekamatwa na maafisa wa shirika la utunzaji wa mazingira nchini NEMA kwa hatia ya kwendeleza  uuzaji wa mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku na serikali nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuwasaka wale wanaokiuka  marufuku hiyo, mkurugenzi wa shirika la NEMA kaunti ya Mombasa Stephen wambua amewaonya watengenezaji, wauzaji na watumizi wa mifuko ya plastiki kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Kwa upande wake katibu wa mazingira kaunti ya Mombasa Godfrey Nato, amesema wameanzisha oparesheni ya pamoja ya kuwasaka wote wanaotumia mifuko hiyo inayochangia pakubwa katika uchafuzi wa mazingira.

Show More

Related Articles