HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

UPI MWELEKEO NASA? : Hasa baada ya Kalonzo,Mudavadi na Wetangula kususia uapisho?

Muungano wa NASA sasa unaonekana kusambaratika kutokana na ukosefu wa umoja haswa baada ya vinara wake watatu ambao ni kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka, mwenzake wa ANC Musalia Mudavadi na Moses Wetang’ula wa Ford Kenya kutoshiriki kwenye uapisho Jumanne .
Hatua hii imeanzisha safari ya siasa za mwaka wa 2022 kwa vinara hawa na upinzani kwa ujumla baada ya baadhi ya viongozi katika chama cha ODM kumshawishi Odinga kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa viongozi wengine badala ya vinara hao watatu .
Mwanahabari wetu Daniel Kariuki anatathmini mweleko wa NASA huku siasa za mwaka wa 2022 zikianza rasmi.

Show More

Related Articles