HabariMilele FmSwahili

Vurugu katika shule ya upili ya Jamuhuri zamwacha mwanafunzi mmoja hali mahututi

Mwanafunzi mmoja yuko hali mahututi katika hospitali ya Kenyatta kufuatia vurugu katika shule ya upili ya Jamhuri. Kulingana na afisa kutoka idara ya kukabili majanga Bramuel Muhongo wanafunzi wengine 15 wamelazwa katika hospitali ya Guru Nanak. Nne kati yao wanaarifiwa kudungwa visu wakati wa vurugu hizo. Mwalimu mkuu Fred Awour pia alijeruhiwa. Baadhi ya wanafunzi wameelezea kuwa vurugu hizo zilianza jumatatu wiki hii baina ya wanafunzi wawili wa kidato cha kwanza na cha nne. Mkuu wa polisi kaunti ya Nairobi Japhet Koome anaongoza uchunguzi kuhusiana na kisa hicho wakati huu.

Show More

Related Articles