MichezoPilipili FmPilipili FM News

Bongwe United Yawatifulia Vumbi Bambini Fc

Timu ya Bongwe united imeibuka na ushindi wa bao 2 dhidi ya ya Bambini Fc katika mchuano wa finali za ukunda super cup .

mtinange huo uligaragazwa katika  uwanja wa maonyesho  ya kilimo ya ukunda  ambapo Mchezaji Yusuf Vitoto wa timu ya bongwe united alichana nyavu kunako  dakika ya 19 kwenye kipindi cha kwanza  cha ngarambe hio, huku Idd Njama akiipatia bao la pili mnamo dakika ya 37 ya kipindi hicho.

Bongwe united wamejizolea kitita cha fedha cha shilingi elfu 20 , sare za jezi na kombe lililodhaminiwa na waziri  wa utamaduni , michezo ,jinsia ,vijana na maendeleo ya jamii kaunti ya kwale Ramadhan Masoud Bungale .

Show More

Related Articles