HabariPilipili FmPilipili FM News

Mganga Atiwa Mbaroni, Mkongani Kaunti Ya Kwale

Wakaazi wa wadi ya mkongani kaunti ya Kwale wanatishia kuandamana  hadi  katika mahakamani   ya kwale kupinga kufunguliwa mashtaka  kwa mganga mmoja kwa jina omar mboni  aliyekuwa akitekeleza oparesheni ya kuwakamata washukiwa wa uchawi katika vijijini 13 vya wadi hio.

Mganga huyo alikamatwa na maafisa wa polisi  siku ya jumapili katika kijiji cha mkomba huko mkongani akitekeleza operasheni yake katika boma la mzee abdallah musa nyangasi anayedaiwa na wenyeji kuwa mchawi  baada ya mzee huyo kujisalimisha katika kituo cha polisi cha burani baada ya wakaazi waliojawa na ghadhabu kutishia kumuangamiza.

Naibu kamishna eneo la matuga benson maisori amesema mganga huyo anadaiwa kuchukua jumla ya shilingi 650,000 kutoka kwa wenyeji wa vijiji ili kukamatiwa wazee wanaodai kuwa na vitendo vya  kichawi wanavyotaja kusambaratisha maendeleo katika vijiji hivyo hususan elimu na maafa miongoni mwa mwenyeji.

Hata hivyo amedokeza kuwa wamemkamata mganga huyo kwa kutekeleza shughuli zake kinyume cha sheria na kuhatarisha maisha ya wazee katika eneo hilo akisema kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi mjini kwale na atafikishwa mahakamani leo kufunguliwa mashtaka kuzua taharuki ,  kutuhumu wazee kuwa wachawi na kuhatarisha maisha yao

Show More

Related Articles