HabariMilele FmSwahili

KUPPET yataka rais Kenyatta kukamilisha kutaja baraza la mawaziri ili kubaini atakayekuwa waziri wa elimu

Chama cha KUPPET kimemtaka rais Uhuru Kenyatta kukamilisha shughuli ya kutaja baraza lake la mawaziri ili kuweza kubaini atakayekuwa waziri wa elimu. Mwenyekiti wa KUPPET Amboko Milemba ambaye ni mbunge wa Emuhaya anasema hali ilivyo kwa sasa inaathiri baadhi ya shughuli za elimu. Licha ya kumkosoa kaimu waziri wa elimu Fred Matiangi na tume ya kuwajiri walimu nchini TSC kwa uhamisho wa wakuu wa shule amewataka wenyeji wa Emuhaya kutowafurusha wakuu watakaotumwa katika shule zilizoko sehemu hiyo. Hata hivyo anasisitiza shughuli hiyo ingeendeshwa kwa umakini kutokana na migawanyiko iliyoko nchini kwa sasa.

Show More

Related Articles