HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa Mwatate Watarajiwa Kupokea Hatimiliki Za Mashamba yao

Huenda wakaazi wa mtaa wa Mwatate kata ya Chaani gatuzi dogo la Changamwe kaunti ya Mombasa wakanufaika na mradi Kenya Informal Settlement Improvement Project (KISIP) wenye malengo ya kuboresha mtaa huo wa makazi duni.

Akiongea na wanahabari mzee wa mtaa Andrew Angusi amesema mradi huo utawasaidia pakubwa ikizingatiwa kwamba kutawekwa miundo msingi bora na nyumba za kudumu.

Angusi amedokeza kuwa lakufurahisha zaidi ni kuwa wale wote wenye nyumba watapata hatimiliki.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya wanakijiji hicho Vick Mwendwa amesema kuwa kwenye kikao na wadau hao mchakato huo unafikia hatua za mwisho.

Show More

Related Articles