HabariPilipili FmPilipili FM News

Alfred Mutua Amtaka Rais Uhuru Kuzingatia Usawa Katika Ugavi Wa Nyadhfa Serikalini

Huku rais Uhuru Kenyatta akitarajiwa kukamilisha uteuzi wa baraza lake la mawaziri hivi karibuni , viongozi wa chama cha maendeleo ChapChap mojawapo wa chama tanzu katika serikali ya jubilee wamemtaka rais  kuzingatia usawa wakati wa ugavi wa nyadhfa mbalimbali serikalini, ikiwemo uteuzi wa mawaziri, mabalozi na hata wajumbe wa kamati mbalimbali za bunge.

Hayo ni kwa mujibu wa kinara mkuu wa chama hicho aliyepia gavana wa Machakos Alfred Mutua.

Kuhusu mazungumzo ya kitaifa yanayoshinikizwa kati ya mrengo wa jubilee na NASA, Mutua amesema mazungumzo hayo yanapaswa kushirikisha viongozi wote na wananchi kwa ujumla, na wala sio viongozi wachache kutoka mirengo miwili ya kisiasa.

Akiongea katika makao makuu ya chama cha maendeleo Chap chap jijini Nairobi ,gavana Mutua aidha amemtaka rais Kenyatta kuwakabili wafisadi katika muhula wake wa pili na wa mwisho, akisema ufisadi umechangia matatizo mengi kwa wakenya.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker