HabariMilele FmSwahili

Matiangi: Mpango wa kuwahamisha walimu wakuu utaendelea licha ya pingamizi

Mpango wa kuwahamisha walimu wakuu utaendelea licha ya pingamizi. Ni kauli ya waziri wa elimu Dkt Fred Matiangi ambaye pia amewaonya vikali baadhi ya viongozi wanaopinga uhamisho huo kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria. Kulingana na Matiangi baadhi ya viongozi hao wamekuwa wakizuia uhamisho kutokana na kutaka kuficha ukweli kuhusu maovu yakiwemo ubadhilifu wa fedha za mashule. Matiangi pia amewataka wenye pingamizi kuwasilisha ushahidi wao kwa tume ya kuwaajiri walimu badala ya kuchukuwa hatua mikononi. Wakati huo huo Matiangi ameelezea kutoridhishwa na idadi ndogo ya wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza katika eneo la Pwani wiki hii. Matiangi amemtaka mshirikishi wa kanda ya Pwani Nelson Marwa kubaini chanzo cha tatizo hili na kuhakikisha wanafunzi wote wanajiunga na shule.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker