HabariSwahili

Wenyeji walalamikia kudorora kwa usalama katika mpaka wa Kuria na Trans Mara Mgharibi

Wenyeji wanaoishi kwenye mpaka wa Kuria na Trans Mara Magharibi wamelalamikia vikali kudorora kwa hali ya usalama mpakani humo. Wakiongozwa na Jonathan Lerionka, wanasema magenge yenye silaha kali yamekuwa yakiwahangaisha, hali ambayo imewatia hofu. Wenyeji hao pia wamelaani tukio la jana ambapo watu wasiojulikana walivamia kituo cha kibiashara cha Enoosaen na kupora pesa na mali ya dhamani kubwa. Chifu John Ole Naleke hata hivyo anasema uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na kisa hicho huku akiongeza kuwa usalama umeimarishwa

Show More

Related Articles