People Daily

Shirika La Ferry La Pania Kuongeza Huduma Zake

Shirika la huduma  za Ferry nchini linapania kuongeza huduma zake katika vivuko vya ziwa Victoria na Turkana, pamoja na kuanzisha safari za baharini kutoka eneo la shimoni kaunti ya Kwale hadi kaunti ya Lamu.

Akitoa kauli hiyo mwenyekiti wa shirika hilo Ramadhan Seif Kajembe amesema lengo kuu la mpango huo ni kuhakikisha kila mkenya anapata huduma bora za usafiri.

Wakati huo huo amesema pia wanaweka mipango zaidi ya kuanzisha uchukuzi wa baharini kutoka kaunti moja hadi nyingine kanda ya pwani, hiyo ikiwa njia moja ya kupunguza visa vya uhalifu ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa barabarani.

Show More

Related Articles