HabariMilele FmSwahili

IPOA yaanzisha uchunguzi kuhusu madai ya mtu mmoja kuwawa na polisi Suswa Narok

Mamlaka ya kuangazia utendakazi wa polisi IPOA imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya mtu mmoja kuuwawa kwa kupigwa risasi na afisa wa polisi eneo la Suswa kaunti ya Narok wiki iliyopita. Katika taarifa IPOA inasema imeanza kupokea ushahidi kabla ya kuchukuwa hatua dhidi ya afisa wa polisi aliyehusika. Kisa hicho kilijiri baada ya kundi la zaidi ya vijana 100 kuvamia kituo cha SGR wakitaka kuajiriwa hali iliyopelekea makabiliano baina yao na polisi. Wakati uo huo mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya ardhi Dr Mohamed Swazuri anazuru eneo la duka moja leo ambapo atapokea lalama za wenyeji hao wanaodai fidia kwa ardhi zao zilizotwalia kwa ujenzi wa reli ya kisasa

Show More

Related Articles