HabariPilipili FmPilipili FM News

Huduma Katika Kivuko Cha Ferry Ya Mtongwe Zarejelea

Huduma katika kivuko cha ferry ya mtongwe zimerejea kawaida baada ya kusimama kutoka mwezi wa Oktoba Mwaka Jana.

Sasa huduma hiyo itatekelezwa kwa zamu, ya kwanza ikiwa nikutoka alfajiri hadi saa nne asubuhu huku ya pili ikiwa ni kutoka saa kumi alasiri hadi saa nne usiku.

Bakari Gowa ambaye ni mkrugenzi mkuu wa huduma za ferry nchini amewaomba msamaha wakaazi wa Mtongwe kwa mahangaiko waliopitia kwa mda huo ferry haikuwa ikihudumu na kutoa hakikisho kwamba watafanya kadri ya uwezo wao ili kufanikisha huduma hiyo.

Baadhi ya wannchi tuliozungumza nao wameonyesha kufurahishwa na huduma hiyo kurejea na kuliomba shirika la ferry kuhakikisha kuwa wamepokea huduma hiyo kwa masaa 24  kama ilivyo katika kivukio cha Likoni

Huduma za ferry ya Mtongwe zilizinduliwa upya mwaka jana na rais Uhuru Kenyatta, baada ya shughli katika kivukio hicho kusitishwa kwa zaidi ya miaka 20 kutokana na mkasa uliotokea ambapo mv Mtongwe ilizama na watu zaidi ya mia mbili wakaangamia.

Show More

Related Articles