HabariMilele FmSwahili

Mahakama ya Homabay yatupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wa mbunge Tom Odege

Mbunge wa Nyatike Tom Odege ana kila sababu ya kutabasamu baada ya mahakama kuu ya Homabay kutupilia mbali kesi ya kupinga ushindi Wake. Jaji Joseph Karanja amesema mlalamishi Fredrick Odiso hakuwasilisha sababu za kutosha kupinga ushindi wa Odege. Akizungumza katika majengo ya bunge mchana huu Odege amewarai wapinzani wake kumpa muda wa kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo kuinua viwango vya elimu.

Show More

Related Articles