HabariMilele FmSwahili

Serikali kufanyia mabadiliko uwanja wa ndege wa JKIA siku 100 zijazo

Serikali itafanyia mabadiliko uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kuimarisha utoaji huduma katika muda wa siku 100 zijazo. Mawaziri Dr Fred Matiangi wa usalama, James Macharia wa uchukuzi na Najib Balala wa utalii waliozuru ghafla eneo hilo leo wanasema ni sharti uwanja huo ambao ni kioo cha taifa uafikie viwango vya juu ili kuwavutia wawekezaji. Waziri Matiangi amewapongeza maafisa wa usalama kwa kutekeleza wajibu wao japo amewataka kujikakamua zaidi waziri wa utalii Najib Balala naye anasema wote wanaofanya kazi uwanjani humo ni sharti wapokee mafunzo ya uhusiano mwema kutoka taasisi ya utalii

Show More

Related Articles