BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Musa Babaz Ni Meneja Muongo Asame Chikuzee.

Kila mwaka una vijimambo vyake kwani mwaka huu umeanza na vituko vya kiaina yake.

Msanii Abdallah Chikuku alimaarufu Chikuzee mwaka wake umeanza kwa kutangaza rasmi kuachana na meneja wake wa muda mrefu Musa Babaz ambaye wengi tulijua wangedumu pamoja katika tasnia ya mziki.

Lakini sasa Chikuzee ambaye anatamba na ngoma yake mpya ya Usiondoke aliyomshirikisha msanii wakufoka kutoka Tanzania Stamina ameweka wazi kwamba yeye na Musa Babaz hali si njema kwani aliyoyategemea kuyapata kutoka kwa Babaz yalikua ndoto tu.

“Nilisubiri sana kwa muda mrefu meneja wangu anifanyie vitu vingi kwa mfano anisaidie kurekodi ngoma nyingi na kunitolea video nzuri lakini wapi,aliniahidi gari nikasubiria but ilikua bure tu mafans wangu wakaniona nimefifia kimziki na sasa ni meamua nianze mziki kivyangu sitaki kusimamiwa tena”. Amesema Chikuzee alipokua akihojiwa ndani ya MwakeMwake Live na Gates.

Wakati huohuo msanii huyo amedokeza kuwa Musa Babaz ni meneja muongo ambaye huezi mwamini akufanyie vitu vyako kwa wakati na ameitaja kuwa sababu kubwa ya yeye kupotea kimziki ila akaahidi kujipanga upya na karibuni atabwaga mizigo mizito.

Lakini baada ya meza ya soga za usanii kuongea na meneja Musa Babaz moja kwa moja katika studio za Pilipili Fm kwenye kipindi cha Mwake Mwake Live alikana madai hayo ya Chikuzee akimtaja msanii ambaye anakosa fadhila kwani alikua anaishi nay eye kama motto wake na ndugu yake hivyo hapaswi kujitoa kwa Media nakuanza kumhukumu vibaya.

“Chikuzee ni msanii asiye na shukrani Gates kwa sababu mimi nilimchukua na kumlea nikamsimamia but kama anadhani sijamfikisha mbali kimziki ni sawa ila anakosea kujitokeza kwa vyombo vya habari angenambia mwenyewe tujue makosa yako wapi ila sawa tu Mungu atalipia mimi sina lakuongezea namtakia kila la kheri kwa sababu ni msanii mzuri na mkubwa Afrika mashariki “.Amesema Babaz kwa hasira.

Hayo ndio mambo ambayo yamejiri katika mwezi wa kwanza wa mwaka huu wa 2018.

 

Show More

Related Articles