People Daily

Wakaazi Wa Kwale Walalamikia Uhaba Wa Maji

Baadhi ya viongozi kwale wanasema kuwa wako tayari kuungana na wakaazi kufanya maandamano makubwa ya kushinikiza usimamizi wa kampuni ya huduma za maji kuachilia maji kwa Wananchi au mkurugenzi wa kampuni hio abanduke mamlakani .

Hii imeibuka katika kikao cha ukusanyaji maoni ya Wananchi ya makadirio ya bajeti ya mwaka 2018/2019  eneo la Kombani ambapo wakaazi  wakiongozwa na Juma Mwakutsinza wamelalamikia uhaba mkubwa wa maji kwale kila mwaka  licha ya kuwa vyanzo vikuu vya maji vinapatikana katika kaunti hio.

Mwakilishi wa wadi ya Waa-ng’ombeni  Mwinyi Mwasera na mjumbe maalum Mishi Mayumbe wanasema kila mwaka katika makadirio ya bajeti wakaazi wamekuwa wakilalamikia swala la maji na hakuna mabadiliko yoyote katika kampuni hiyo.

Hata hivyo afisaa  katika kampuni ya maji Katana Antony Katana ameitetea kampuni hiyo akisema haina ufisadi ila sheria ya usimamizi wa maji bado haijakua wazi.

Show More

Related Articles