HabariPilipili FmPilipili FM News

Hitilafu Ya Umeme Ya Sababisha Giza Kote Nchini

Maeneo mengi humu nchini jana jioni yaligubikwa na giza baada ya umeme kupotea kwa masaa mengi kufuatia hitilafu kubwa katika kituo cha kusambaza nguvu za umeme  humu nchini.

Kulingana na taarifa ya kampuni ya Kenya Power maeneo yaliyoathirika kwa takriban saa saba ni kaunti Mombasa, Nairobi, Nyeri, Embu, Bomet , Nyandarua miongoni mwa kaunti nyingine.

Hata hivyo wahandisi wa kampuni ya KPLC waliweza kudhibiti hali hiyo na stima zilirudi majira ya saa saba usiku wa jana

Show More

Related Articles