HabariMilele FmSwahili

Seneta Gideon Moi akana madai anashawishi uteuzi wa baraza la mawaziri

Seneta wa Baringo Gideon Moi amekana madai anashawishi uteuzi wa baraza la mawaziri unaoendeshwa na Rais Uhuru Kenyatta na naibu rais EWilliam Ruto. Moi anasema hajashiriki kwa namna yeyote kwenye uteuzi huo na kutaja madai hayo kuwa propaganda. Akiongea katika majengo ya bunge, seneta Moi amesema ni jukumu la rais na naibu wake kuchagua mawaziri bila mwingilio wa yeyote. Aidha amekanusha madai yuko tayari kuteuliwa kama waziri akisema kwa sasa anaangazia kuhudumu kama seneta wa Baringo.

Show More

Related Articles