People Daily

Chikungunya Ya zidi Kutanda Changamwe

Hali ya wasi wasi ingali imetanda katika mitaa mingi eneobunge la changamwe kutokana na jinsi ugonjwa wa chikungunya unavyo sambaa kwa haraka.
Safiya Dima ambaye ni mwathiriwa na mkaazi wa eneo hilo, anasema kufikia sasa karibu majirani zake wote wameathirika na ugonjwa huo,ambapo hofu yake kuu ni kuwa madakitari wengi bado hawana ufahamu wa kutosha kutibu maradhi hayo.
Ameiomba serikali ya kaunti kufanya utafiti wa kina kubaini chanzo halisi cha ugonjwa huo akisema huenda ikawa chanzo chake sio mbu kama inavyodhniwa.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya gavana wa kaunti ya mombasa Hassan Ali Joho kuzindua mashine tano , ambazo zitatumiwa kufukiza dawa katika maeneo yaliyoathirika zaidi na kesi za ugonjwa huo, ikiwemo maeneo bunge ya changamwe na likoni

Show More

Related Articles