HabariMilele FmSwahili

Serikali yaanza ujenzi wa mabwawa 58 katika kaunti kame kote nchini

Serikali imeanzisha ujenzi wa mabwawa 58 kote nchini kukabili athari za ukame. Mabwawa hayo yatajengwa katika kaunti kame ambako wakazi wameathirika zaidi kutokana na ukosefu wa maji. Katibu wa wizara ya maji Profesa Fred Segor amesema hatua hiyo inafuatia utabiri wa idara ya hali ya anga kuwa ukame utakithiri zaidi nchini mwaka huu. Amesema hayo katika hafla ya uzinduzi wa bwawa la Kimoi ambalo liligharimu shilingi milioni 21 na litarajiwa kuwafaidi zaidi ya wakazi 2000 wa Baringi ambao hutaabika kutokana na ukosefu wa maji.

Show More

Related Articles