HabariPilipili FmPilipili FM News

kitengo cha maji  Cha Tengewa Fedha Zaidi Katika Kaunti Ya Taita Taveta

Serikali ya kaunti ya kwale imeanzisha  rasmi zoezi la kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu makadirio ya bajeti ya mwaka 2018/2019 ya Shilingi bilioni 8.29.

Zoezi hilo limeng’oa nanga katika kila eneobunge la kaunti hiyo lengo kuu ikiwa kutoa mwongozo wa jinsi fedha hizo zitakavyotumika kwa miradi ya Maendeleo.

Afisa msimamizi wa kamati ya bajeti Antony Kalama anasema Bilioni 4.06 amabyo ni sawa na asilimia 48.9% zitaenda kwa miradi ya Maendeleo huku bilioni 4.23 ambazo ni sawa na asilimia 50.06 zikielekezwa  kwa bajeti ya kujaliza mahitaji mengine ya kaunti.

Hata hivyo kitengo cha maji  kimepewa kipaumbele na kutengewa kima cha Shilingi milioni 838.42  ikifuatiwa na idara ya barabara iliyotengewa Shilingi milioni 823.8.

Katika makadiro hayo ya bajeti idara ya afya katika kaunti hiyo imetengewa Shilingi milioni 587.14.

Show More

Related Articles