People Daily

Madereva Wa Uber WaLalamikia Kunyanyaswa Na Polisi

Wahudumu wa magari ya teksi za uber wanaendeleza mgomo baridi kutokana na kile wamekitaja kama kunyanyaswa na maafisa wa polisi, hususan katika kituo cha reli ya kisasa eneo la Miritini.

Wakiwasilisha lalama zao mbele ya kamanda wa polisi wa Kituo hicho Marcella Andaje, Madereva hao wamewalaumu polisi kwa kulemaza shughuli zao kwa kile wanadai maafisa hao wamekuwa  wakiwazuia kuingia katika kituo hicho kuchukua abiria.

Kwa upande wake Andaje ameahidi kuwekwa mipangilio maalum ambayo itatumiwa na madereva hao kurahisisha uchukuzi katika hali ambayo haitatatiza shughuli nyinginezo.

Show More

Related Articles