HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Majina ya mawaziri wapya walioteuliwa yawasilishwa bungeni

Majina ya mawaziri walioteuliwa na Rais Uhuru Kenyata mwishoni mwa juma lililopita sasa yamefikishwa bungeni tayari kupigwa msasa.

K24 imebaini kwamba kuanzia kesho wakenya watakuwa na muda wa siku saba za kutoa maoni yao kuhusiana na uteuzi wa watatu hao John Munyes, Keriako Tobiko na Ukur Yattani na kisha kutoa nafasi kwa bunge kuwapigia msasa na kuandika ripoti katika kipindi cha siku saba zingine.

Hhuenda baadhi ya mawaziri kati ya kumi na tatu waliodaiwa kutemwa wakajipata ndani ya baraza la mawaziri lakini katika wizara tofauti.

Show More

Related Articles