HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Shule ya Starehe Boys yasema haitatoa nafasi kwa wanafunzi wa kutwa

Usimamizi wa shule ya upili ya Starehe Boys Center umetangaza kwamba hautakubali wito wa serikali unaowataka kuwasajili wanafunzi wa kutwa katika kidato cha kwanza mwaka huu.

Kulingana na Mkurugenzi wa shule hiyo Charles Masheti, mtindo na mwongozo unaosimamia shule hiyo hautoruhusu Starehe Boys kuwasitiri wanafunzi wa kutwa kwa kuzingatia hatari ya wanafunzi kuhusika matumizi ya dawa za kulevya na mienendo mingine isiyofaa.

Hata hivyo, shule hiyo imeendelea kuwasajili wanafunzi wapya wa bweni katika kidato cha kwanza.

Show More

Related Articles