HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Robert Godec ataka NASA na Jubilee kufanya mazungumzo

Balozi wa Marekani nchini Robert Godec amesisitiza haja ya mazungumzo baina ya wana NASA na Jubilee ili kutatua mgogoro wa kisiasa uliomo.

Godec anasema hakuna uwezekano wa uchaguzi mkuu chini ya siku tisini na hivyo linalosalia ni kwa washikadau wakuu kuharakisha juhudi za mazungumzo ya kitaifa.

Hata hivyo uongozi wa walio wachache katika mabunge yote mawili umesisitiza kwamba mipango ya kumwapisha Odinga tarehe thelathini Januari haitazuiliwa hadi pale kutakuwa sababu tosha kuisitisha.

Show More

Related Articles