HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanawake Zaidi Hufa Kutokana Na Magonjwa Ya Moyo

Utafiti wa hivi karibuni umeonyesha Ni wamawake wachache ambao hupatwa na matatizo ya mshtuko wa moyo wanaoweza kufariki ikiwa watapata matibabu sawa na yale wanayopewa wanaume.

Utafiti huo uliangazia matokeo ya wagonjwa 180,368 nchini uswizi, ambao walikabiliwa na mshtuko wa moyo katika kipindi cha miaka 10.

Utafiti huo pia umefichua kuwa wanawake wako kwenye hatari kubwa ya  kufariki kutokana na mshtuko wa moyo kuliko wanaume wanapopatwa na hali hiyo.

Kulingana na British Heart Foundation,  mshtuko wa moyo mara nyingi huonekana kama tatizo la wanaume lakini wanawake zaidi hufa kutokana na magonjwa ya moyo hata kuliko saratani.

Show More

Related Articles