HabariMilele FmSwahili

Wauguzi kaunti ya Siaya watishia kugoma

Wauguzi kaunti ya Siaya sasa wanatishia kugoma ifikiapo kesho iwapo hawatakuwa wamelipwa mishahara yao ya miezi 9 iliyopita. Katibu wao Sylvester Ng’anda anasema kaunti ya Siaya iliyokuwa imeahidi kutoa mishahara yao ijumaa iliyopita japo hilo halikutendeka. Anasema iwapo kesho jioni fedha zao hazitakuwa katika akaunti zao hawatakuwa na budi ila kusambaratisha utoaji huduma.

Show More

Related Articles