HabariMilele FmSwahili

Mpango wa elimu bila malipo kuanza kutekelezwa katika shule za sekondari nchini kesho

Mpango wa elimu bila malipo utaanza kutekelezwa katika shule za Sekondari nchini kesho ambapo wanafunzi wa kidato cha kwanza wataripoti shuleni. Kulingana na katibu wa wizara ya elimu Dkt Belio Kipsang serikali imetenga shilingi bilioni 29.5 kufadhili elimu ya wanafunzi hao ya bila malipo. Kipsang pia amedhibitisha kutolewa kasi kingine cha shilingi bilioni 7.5 kufanikisha uswambazaji wa vitabu kila mwanafunzi anayejiunga na kidato cha kwanza akitarajiwa kupokea vitabu sita vya masomo ya hesabati,kiingereza kiswahili kemia na biolojia.

Show More

Related Articles