HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwakilishi Wa Wadi ataka shisha Ihalalishwa kaunti ya Mombasa

Mwakilishi wadi mteule Fatuma Kushe anatarajiwa kuwasilisha mswada katika bunge la kaunti ya Mombasa wa kutaka Shisha iuzwe katika maeneo kadhaa baada ya kibali cha kuuza shisha kutolewa na serikali ya kaunti.

Kushe anasema marufuku ya uvutaji shisha inakiuka haki na faragha ya watu huku akisema huduma ya afya imegatuliwa na serikali za kaunti zina jukumu kuhusiana na suala hilo.

Aidha ameitaka serikali pia kupiga marufuku utumizi wa vileo vingine badala ya shisha pekee

Show More

Related Articles