People Daily

Alphones Baya Akula Kiapo Kama Askofu Wa ACK Mombasa

Hatimaye Alphonce Baya Mwaro ndie askofu mpya wa kanisa la kianglikana Almaarufu ACK hapa mjini Mombasa baada ya kuapishwa katika sherehe za Kihistoria zilizofanyika katika awanja wa Mbaraki hapa mjini Mombasa.

Akihutubia waumini wa kanisa hilo Baya amesema kuwa atadumisha uhusiano mwema na kuendeleza ushirikiano wa kanisa na jamii katika eneo hili.

Baya aliapisha Kwenye sherehe zilizohudhuriwa na maaskofu mbalimbali pamoja na wanasiasa siku chache tu baada ya mahakama kuu ya Mombasa kuamuru kuapishwa kwake.

Askofu huyo anatarajiwa kuhudumu kama Askofu Mkuu wa kanisa hilo mpaka kustaafu kwake atakapo kuwa na miaka 65, Novemba 22 Mwaka 2043.

Show More

Related Articles