People Daily

Wanafunzi Watakaojiunga Na Shule Za Upili Wapata Ufadhili Kwale

Jumla wanafunzi 200 kaunti Kwale watakaojiunga na shule za upili za bweni wamepata ufadhili kutoka kwa  kampuni ya uchimbaji madini ya base titanium.

Akizungumza na wazazi na wanafunzi katika halfa ya   kuzawadi shule kumi bora maarufu host schools zilizofanya vyema katika mtihani wa kcpe katika eneo la mafisini huko msambweni, afisa wa shirika la  base titanium Juma Lumumba,amesema wamesitisha mpango wa kuwalipia wanafunzi wa shule za kushinda za upili kutokana na mpango wa serikali wa elimu bila malipo kwa shule za upili za kutwa.

Lumumba akiwataka  wazazi wa wanafunzi  waliopata ufadhili kugharamia sare za  shule za watoto wao  pamoja na mahitaji madogomadogo.

Show More

Related Articles