HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Shughuli za matibabu hospitalini St Mary’s Nakuru zakwama

Mzozo wa uongozi  unazidi kushuhudiwa katika hospitali ya kimisheni ya St. Mary’s  baina ya Watawa wa Assumption of Sisters of Nairobi na Padre William Fryda  kutoka uingereza,  huku  hii leo  huduma za matibabu zikitatizika  katika mojawapo ya hospitali hizo iliyoko katika eneo la Elementaita kaunti ya Nakuru .
Hali hiyo ikionekana kuwa mbaya pale wafanyikazi katika hospitali hiyo waliripotiwa kuiba vifaa vya hospitali kama njia mojawapo ya kupinga  kutwaliwa kwa lazima  uongozi wa hospitali hiyo na watawa hao, baada yao kupata kibali cha mahakama kama wamiliki halisi wa hospitali hiyo na ile ya Lang’ata jijini Nairobi.

Show More

Related Articles