HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Rais Kenyatta asalia na mawaziri 6 pekee katika baraza la sasa

Hatima ya mawaziri kumi na watatu kwenye baraza la mawaziri imebaki kuyumbayumba baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuwatema kutoka kwa baraza la mawaziri kwenye awamu ya pili ya uongozi wake na kusalia na sita waliokuwa kwenye baraza hilo huku waziri Fred Matiangi akipata uhamisho hadi wizara ya usalama wa ndani na saa kuwa kaimu waziri wa elimu.
Baadhi ya mawaziri wakiwa wale walichangia sana kwenye serikali hapo awali akiwemo Waziri wa Ugatuzi Mwangi Kiunjuri, Waziri wa Maji Eugene Wamalwa na mwenzake wa Masuala ya Kigeni Amina Mohamed, Waziri wa Afya Cleopa Mailu na Waziri wa Ardhi Jacob Kaimenyi ni miongoni mwa wale waliotemwa.

Show More

Related Articles