Pilipili FmPilipili FM News

Mwanaume Mmoja Afariki Baada Ya Kugongwa Na GariMoshi

Mwanaume mmoja mwenye umri wa makamo amefariki dunia baada ya kugongwa na garimoshi katika kijiji cha Bogobogoni eneo bunge la changamwe

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 37 kwa jina Michael Nyamai anakisiwa kuwa mlevi wakati aliopokutana na ajali hiyo usiku wa kuamkia leo.

Kulingana na Magret Nyagasi ambaye ni mzee wa mtaa eneo hilo, takriban watu 6 wamefariki katika siku za hivi karibuni kutokana na ajali za kugongwa na garimoshi eneo hilo huku chanzo kikiwa ni ulevi.

Wito umetolewa kwa wakaazi wa eneo hilo kuepukana na  reli iyo pale wanapokuwa walevi masaa ya usiku ili kuepuka maafa zaidi.

Show More

Related Articles