HabariMilele FmSwahili

Serikali kuzindua mchakato wa usambazaji vitabu vya mtaala mpya wa elimu leo

Serikali itazindua leo mchakato wa usambazaji vitabu vya mtaala mpya wa elimu nchini. Rais Uhuru Kenyatta ataanzisha msafara wa kusambaza vitabu hivyo katika hafla inayoandaliwa hapa Nairobi. Waziri wa elimu Dkt Fred Matiangi wachapishaji na wadau katika sekta ya elimu pia watahudhuria hafla hiyo. Vitabu hivyo vinavyofadhiliwa na serikali vitasambazwa moja kwa moja katika mashule. Hii ni baada ya serikali kutangaza sera mpya ya kuzuia usambazaji vitabu kupitia madalali ili kuepuka hasara.

Show More

Related Articles